Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 1 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 3 2025-01-28

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itatenga fedha za kujenga Daraja la Kijiji cha Lihale na Lusonga katika Mto Ruvuma, ili kuunganisha Mbinga Vijijini na Peramiho?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na kazi za upembuzi yakinifu katika Daraja la Lusonga katika Mto Ruvuma, ili kujenga daraja kubwa la kudumu. Aidha, katika mpango na bajeti ya Mwaka wa Fedha 2025/2026, Serikali imeweka katika mipango yake ujenzi wa daraja la waenda kwa miguu (suspension foot bridge) na pikipiki kwa gharama ya shilingi milioni 175.