Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 132 2025-02-06

Name

Dr. Jasson Samson Rweikiza

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Vijijini

Primary Question

MHE. DKT. JASSON S. RWEIKIZA aliuliza:-

Je ni lini Tanzania itaridhia Mkataba wa Kimataifa wa Kujikinga na Bidhaa za Nyuklia?

Name

Prof. Adolf Faustine Mkenda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Rombo

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU K.n.y. WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Jasson Samson Rweikiza, Mbunge wa Bukoba Vijijini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inatarajia kukamilisha mchakato wa kuridhiwa kwa Mkataba wa Kimataifa wa Kujikinga na Bidhaa za Nyuklia kabla au ifikapo tarehe 30 Juni, 2025. Aidha, mkataba huo umeshawasilishwa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa ajili ya kufanyiwa uridhiwaji. Ahsante.