Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 8 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 136 2025-02-06

Name

Dr. Josephat Mathias Gwajima

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kawe

Primary Question

MHE. ASKOFU JOSEPHAT M. GWAJIMA aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itaanza Matibabu ya Wagonjwa Wenye Seli Mundu kwa kutumia Crispr Gene Editing Technology?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali wakati wote inafuatilia tiba zote bora kabisa duniani na zinazotumia teknolojia bora na mpya, ikiwemo tiba ya CRISPR Cas 9 Technology (Gene Editing).

Mheshimiwa Spika, CRISPR Cas 9 Technology (Gene Editing) ni tekinolojia ambayo toka imeanza kutumika kwa binadamu ni chini ya miaka miwili sasa. Aidha, wakati wa ziara ya Mheshimiwsa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan Nchini Marekani mwaka 2022 alifuatilia tiba hii. Mwaka 2024 wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Rais aliwakilishwa na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania; na suala hili lilikuwa moja ya ajenda iliyojadiliwa kwenye mikutano ya Waziri Mkuu na taasisi za tiba na teknolojia za Kimarekani, pia wagonjwa waliotibiwa na teknolojia hiyo walishiriki katika vikao hivyo.

Mheshimiwa Spika, mara tu teknolojia hii ya CRISPR Cas 9 Technology (Gene Editing) itakapoanza kutumika rasmi duniani kote kama tiba, sisi tutakuwa miongoni mwa nchi za kwanza kupokea kwani toka mwaka 2022 tumeanza kufanya matayarisho ya wataalam na tekinolojia. Kwa sasa nchini kwetu tiba hii tunatoa kwa kufanya upandikizaji wa uloto, huduma ambayo inafanyika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.