Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 9 Information, Communication and Information Technology Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari 153 2025-02-07

Name

Maimuna Salum Mtanda

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Newala Vijijini

Primary Question

MHE. MAIMUNA S. MTANDA aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga minara ya simu katika maeneo mbalimbali yenye changamoto ya mawasiliano - Newala Vijijini?

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Newala Vijijini linaendelea kunufaika na Miradi ya Serikali kupitia Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ambapo mnamo tarehe 30 Agosti, 2022 Serikali kupitia UCSAF iliingia makubaliano na Kampuni ya Simu ya Halotel kwa ajili ya kujenga mnara wa simu katika Kata ya Chitekete kupitia mradi wa mipakani na maeneo maalum wa Awamu ya Sita ambao ulikamilika na wananchi wananufaika na huduma.

Mheshimiwa Spika, aidha, kupitia Mradi wa Tanzania ya Kidigitali Awamu ya Kwanza ambao mkataba wake ulisainiwa tarehe 13 Mei, 2023, Kata ya Makukwe katika Jimbo la Newala Vijijini, ilijumuishwa na kupata mtoa huduma Kampuni ya Yas (zamani ikijulikana kama TIGO) na kwa sasa Yas wameshapata kibali cha ujenzi na mkandarasi anajiandaa kwenda kuanza ujenzi wa mnara huo. Kwa mujibu wa taarifa za Yas, mnara unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Machi, 2025.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Serikali kupitia UCSAF, itafanya tathmini katika maeneo mbalimbali ya Jimbo la Newala Vijijini ili kubaini maeneo yenye changamoto ya mawasiliano ya simu kama alivyowasilisha Mheshimiwa Mbunge ili kubaini mahitaji halisi na kuyaingiza katika mpango wa kuyafikishia huduma katika utekelezaji wa miradi ijayo ya mawasiliano ya simu kulingana na upatikanaji wa fedha. (Makofi)