Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 18 Sitting 2 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Mifugo 27 2025-01-29

Name

Joseph Anania Tadayo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwanga

Primary Question

MHE. JOSEPH A. TADAYO aliuliza:-

Je, lini mnada wa mifugo uliojengwa Kata ya Kileo - Mwanga utafunguliwa?

Name

Alexander Pastory Mnyeti

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Misungwi

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba mnada wa Mpakani Kileo bado haujafunguliwa kwa kuwa mnada ulihitaji ukarabati wa miundombinu muhimu ya vyoo na sehemu ya kupakilia mifugo ambavyo ni muhimu katika shughuli za mnada. Hata hivyo, ukarabati wa miundombinu hiyo ulikamilika mwezi Oktoba, 2024.

Mheshimiwa Spika, uhamasishaji kuhusu matumizi na kuanza kutumika kwa mnada ulifanyika katika Vijiji vya Kifaru, Kileo na Kivulini ambapo waliweza kupendekeza siku ya Jumatano kuwa iwe siku ya mnada. Aidha, Tarehe 4 Desemba, 2024 ilipangwa mnada uanze rasmi, lakini kulitokea changamoto ya kuharibika kwa miundombinu ya barabara kutokana na mvua kubwa zilizonyesha. Hadi kufikia sasa, jitihada za halmashauri zinaendelea na tayari wamewasiliana na TARURA kwa ajili ya kuona namna ya kurekebisha barabara hiyo. Pindi changamoto hiyo itakapotatuliwa mnada wa Kileo utafunguliwa na kuanza kazi, ahsante.