Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 18 | Sitting 14 | Finance | Wizara ya Fedha | 237 | 2025-02-14 |
Name
Omari Mohamed Kigua
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kilindi
Primary Question
Ushiriki wa Wabunge wenye CPA kwenye Kamati
Kuchukuliwa kama CPE Hours
MHE. OMARI M. KIGUA aliuliza:-
Je, lini Wabunge wenye sifa ya CPA ushiriki wao kwenye Kamati za LAAC, PIC, PAC na Bajeti utachukuliwa kama CPE hours?
Name
Dr. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Magharibi
Answer
WAZIRI WA FEDHA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Mwongozo wa Mafunzo Endelevu ya Kihasibu Tanzania (Continued Professional Development- CPD Guideline) uliidhinishwa na Bodi ya Wakurugenzi ya NBAA na kuanza kutumika rasmi Julai 1, 2020. Mwongozo unatambua mafunzo endelevu rasmi yaani uso kwa uso au ya kielektroniki na mafunzo endelevu yasiyo rasmi ikiwa ni pamoja na kushiriki mikutano ya kiufundi katika tasnia ya uhasibu na ukaguzi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kufuata mwongozo huo na kwa kuzingatia muda unaotumiwa na Waheshimiwa Wabunge wakati wa ushiriki wa mikutano ya Kamati za Bunge na hasa zile zinazohusu masuala ya uhasibu au ukaguzi kama LAAC, PIC, PAC na uchambuzi wa Bajeti ya Serikali, saa zinazotumiwa na Wabunge wenye CPA zinatambuliwa kama ni mafunzo endelevu (CPD hours).
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Mbunge ambaye ni mwanachama wa NBAA ataingia kwenye akaunti yake, atapandisha ratiba ya kikao husika na uthibitisho wa mahudhurio katika mkutano husika ili saa zakezi kuhesabiwa. Hivyo, ni jukumu la mwanachama mwenyewe kuingia kwenye mfumo, na siyo mtu mwingine (third party) na kutoa uthibitisho huo kwenye mfumo wa NBAA.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved