Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 2 Finance Wizara ya Fedha 23 2025-04-09

Name

Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza tozo na kodi za uingizaji wa samaki toka nje ya nchi?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Kamati ya Maboresho ya Mfumo wa Kodi (Task Force on Tax Reforms) katika vikao vyake, inaendelea kupokea mapendekezo yanayowasilishwa na wadau kuhusu maboresho ya mfumo wa kodi, ada na tozo mbalimbali ikiwa ni pamoja na eneo la uingizaji wa samaki kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, tathmini ya kina hufanyika ili kubaini hali ya soko, tabia za walaji, mahitaji, gharama, athari kwa mapato ya Serikali na kuzingatia umuhimu wa kulinda walaji na wafanyabiashara wa ndani ili kuongeza mchango wa thamani katika mnyororo wa uchumi. Hivyo, maamuzi na mapendekezo ya kupunguza tozo na kodi za uingizaji wa samaki kutoka nje ya nchi yatafanywa kulingana na matokeo ya tathmini husika. Ahsante sana.