Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 43 Natural Resources and Tourism Wizara ya Maliasili na Utalii 188 2025-04-30

Name

Robert Chacha Maboto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda Mjini

Primary Question

MHE. BONIPHACE M. GETERE K.n.y. MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga Makao Makuu ya TANAPA katika Halmashauri ya Mji wa Bunda?

Name

Dunstan Luka Kitandula

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mkinga

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imetenga eneo lenye ukubwa wa ekari 41.13 katika eneo la Kunzugu, Kata ya Balili, Mjini Bunda kwa ajili ya ujenzi wa Ofisi za TANAPA Kanda ya Magharibi. Kwa sasa, Serikali imekamilisha zoezi la upembuzi yakinifu na uandaaji wa michoro kwa ajili ya ujenzi wa ofisi hiyo. Kazi ya ujenzi inatarajiwa kuanza kwenye Mwaka wa Fedhaa 2025/2026.