Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 500 2025-06-04

Name

Aida Joseph Khenani

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Nkasi Kaskazini

Primary Question

MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza: -

Je, nini sababu ya Wilaya ya Nkasi kukosa miradi ya kimkakati?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) aliuliza: -

Mheshimiwa Spika, Serikali ilianzisha utaratibu wa kutekeleza miradi ya kimkakati katika Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuziwezesha halmashauri kuongeza mapato ya ndani na kuboresha huduma za kijamii na kiuchumi.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya Nkasi iliibua na kuandaa maandiko ya miradi miwili ya kimkakati ya kuboresha minada mitatu ya kisasa na ujenzi wa hoteli ya kisasa katika Mji wa Namanyere. Maandiko hayo yaliwasilishwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI mwezi Julai, 2020 kwa ajili ya uchambuzi. Aidha, miradi hii ilikosa baadhi ya vigezo ikiwemo umiliki wa ardhi ya maeneo ya miradi na kutofanyika kwa upembuzi yakinifu wa miradi husika.

Mheshimiwa Spika, kwa sasa halmashauri ipo katika hatua za mwisho za ukamilishaji wa vigezo vilivyokosekana wakati wa uchambuzi. Mara baada ya hatua hiyo kukamilika na miradi kukidhi vigezo, Serikali itatafuta fedha na kuanza utekelezaji wa miradi hiyo.