Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 501 2025-06-04

Name

Neema Gerald Mwandabila

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. SHALLY J. RAYMOND K.n.y. MHE. NEEMA G. MWANDABILA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka fedha za ujenzi wa majengo mapya ya Kituo cha Afya cha Kamsamba – Momba?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Kamsamba kilijengwa mwaka 1943 na ni miongoni mwa vituo vya afya kongwe 203 ambavyo Serikali imeviainisha kwa ajili ya ukarabati na kuongeza miundombinu yake.

Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha ukarabati wa hospitali 50 kongwe nchini na baadaye itafanya ukarabati wa vituo vya afya kongwe kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya cha Kamsamba.