Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 503 2025-06-04

Name

Innocent Sebba Bilakwate

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyerwa

Primary Question

MHE. INNOCENT S. BILAKWATE aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka gari la polisi na gari la zimamoto katika Wilaya ya Kyerwa inayopakana na nchi mbili ili kukabiliana na majanga ya moto?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, Serikali kupitia Jeshi la Polisi imepeleka gari jipya moja aina ya Toyota Land Cruiser Pickup kwa Polisi Wilaya ya Kyerwa. Aidha, kwa upande wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Serikali itapeleka gari moja katika wilaya hiyo ikiwa ni mpango wa Serikali wa kusambaza magari ya zimamoto na uokoaji kwa wilaya zote nchini kwa ajili ya kukabiliana na majanga ya moto, ahsante.