Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 505 2025-06-04

Name

Joseph Zacharius Kamonga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ludewa

Primary Question

MHE. NEEMA W. MGAYA K.n.y. MHE. JOSEPH Z. KAMONGA aliuliza: -

Je, jitihada zipi zinafanywa na Serikali kuhakikisha Wilaya ya Ludewa inajengewa miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya umwagiliaji katika Wilaya ya Ludewa ikiwemo upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Skimu za Umwagiliaji za Mbwila hekta 4,000, Iselela hekta 1,800 na Bonde la Mto Ruhuhu lenye ukubwa wa hekta 4,500. Upembuzi huo unatarajiwa kukamilika mwezi Juni, 2025 na kuanza taratibu za kumpata mkandarasi kwa ajili ya ujenzi. Aidha, Tume inaendelea na uchimbaji wa kisima cha umwagiliaji katika Kijiji cha Mangalanyene chenye uwezo wa kumwagilia ekari 123. Kisima hicho kikikamilika kitakuwa na uwezo wa kunufaisha wakulima 80 wa zao la chai.