Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Water and Irrigation Wizara ya Maji 506 2025-06-04

Name

Grace Victor Tendega

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. GRACE V. TENDEGA aliuliza:

Je, nini mkakati wa Serikali kuhakikisha uvunaji wa maji ya mvua unapunguza changamoto ya maji?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Serikali inaendelea kutekeleza mkakati wa uvunaji wa maji ya mvua wa miaka mitano kuanzia mwaka 2022 hadi 2026 kwa kujenga mabwawa kwa lengo la kukabiliana na changamoto za mafuriko na ukame. Pia utekelezaji unaendelea wa mkakati wa uvunaji wa maji ya mvua kandokando ya barabara kwa miaka mitano kuanzia mwaka 2020 hadi 2025 kwa kujenga malambo ambao uliandaliwa mahususi kwa ajili ya kulinda miundombinu ya barabara na reli. Kupitia mikakati hiyo, jumla ya mabwawa 45 yamejengwa katika kipindi cha mwaka 2022 hadi 2025, mabwawa 19 yanaendelea na ujenzi kwenye maeneo mbalimbali nchini.

Mheshimiwa Spika, vilevile katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imetenga zaidi ya shilingi bilioni 5.5 kwa ajili ya kukarabati mabwawa 15 ya ukubwa mdogo na wa kati sanjari kuhamasisiha uvunaji wa maji ya mvua kupitia mapaa ya nyumba hususani kwenye taasisi za umma kama mashule, zahanati, vituo vya afya, hospitali na ofisi mbalimbali.