Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Water and Irrigation Wizara ya Maji 507 2025-06-04

Name

Mwita Mwikwabe Waitara

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Vijijini

Primary Question

MHE. MWITA M. WAITARA aliuliza: -

Je, lini maji kutoka Ziwa Victoria yatafika katika Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vilivyopo Tarime Vijijini?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, nakushukuru, Vijiji vya Sirari, Nyamwaga na Nyamongo vinapata huduma ya majisafi na salama kupitia vyanzo vya chemchem na visima virefu vilivyochimbwa kwenye maeneo hayo. Aidha, katika kuboresha zaidi huduma ya maji katika maeneo hayo, Serikali inatekeleza Mradi wa Miji 28 kutoka Ziwa Victoria kwenda katika Wilaya za Rorya na Tarime ambapo kukamilika kwake utanufaisha pia Kijiji cha Sirari. Mradi huo unatarajiwa kukamilika katika mwaka wa fedha 2025/2026.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali itafanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa miradi ya maji kwa ajili ya kufikisha huduma kwenye vijiji ambavyo havijafikiwa na Mradi wa Ziwa Victoria ikiwemo Vijiji vya Nyamwaga na Nyamongo, ahsante.