Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 508 2025-06-04

Name

Francis Isack Mtinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Iramba Mashariki

Primary Question

MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza:-

Je, lini Serikali itakamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami kilometa 42 barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya Mkalama?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, barabara inayoelekea Makao Makuu ya Wilaya ya Mkalama inaitwa Barabara ya Iguguno Shamba hadi Nduguti yenye urefu wa kilometa 42.6. Ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara hii unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa Serikali imekamilisha ujenzi kwa kiwango cha lami wa kilometa 2.5 katika Mji wa Iguguno. Kwa sasa Serikali inaendelea na taratibu za manunuzi ili kumpata mkandarasi wa ujenzi wa kilometa 10 kwa kiwango cha lami. Kwa sehemu iliyobaki Serikali itaendelea kutafuta fedha ili kuendelea na ujenzi, ahsante. (Makofi)