Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 509 2025-06-04

Name

Benaya Liuka Kapinga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Vijijini

Primary Question

MHE. BENAYA L. KAPINGA aliuliza: -

Je, lini Serikali itaanza upembuzi yakinifu na kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Nyoni – Maguu?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na ujenzi wa Barabara ya Nyoni – Maguu yenye urefu wa kilometa 30.55 kwa kiwango cha lami inafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa kipande cha barabara hiyo chenye jumla ya urefu wa kilometa 5.6 kinachopitia kwenye maeneo korofi yenye miteremko mikali tayari kimejengwa kwa kiwango cha lami na zege, ambapo kwa kilometa 4.6 kimejengwa kwa kiwango cha lami na kipande cheye urefu wa kilometa 1.0 kimejengwa kwa kiwango cha zege. Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kufanya kazi ya upembezi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuijenga barabara yote kwa kiwango cha lami, ahsante.