Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 39 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 510 2025-06-04

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA K.n.y. MHE. HAWA M. CHAKOMA Aliuliza: -

Je, ni lini Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami kutoka Kilindoni – Rasimkumbi - Mafia kilometa 52.16?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI Alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa Barabara ya Kilindoni – Rasimkumbi - Mafia (kilometa 52.16) kwa awamu. Katika mwaka wa fedha 2022/2023 na 2023/2024 Serikali imekamilisha kujenga jumla ya kilometa 2.15. Kwa sehemu iliyobaki (kilometa 50.13) iko katika hatua za manunuzi ya kumpata mkandarasi wa ujenzi.