Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 225 2025-05-06

Name

Mary Francis Masanja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MARY F. MASANJA aliuliza: -

Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa na Watumishi Kituo cha Afya Budushi Wilayani Kwimba?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imeendelea kuajiri watumishi wa Kada ya Afya na kuwapeleka kwenye vituo vya kutolea huduma za afya kote nchini. Katika mwaka wa fedha 2024/2025 jumla ya watumishi 9,384 waliajiriwa na kupangiwa kazi katika vituo vya kutolea huduma katika halmashauri, ambapo jumla ya watumishi 32 wa afya walipangwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba. Kituo cha Afya Budushi kina jumla ya watumishi 12.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilinunua magari 594, ambulances 382 na magari ya usimamizi wa huduma za afya 212, katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Wilaya ya Kwimba imepokea magari matatu ya kubebea wagonjwa na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kwimba, Kituo cha Afya Malya na Kituo cha Afya Kadashi.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa sasa dharura zinazotokea kwenye Kituo cha Afya Budushi zinahudumiwa na gari la kubebea wagonjwa lililopo Hospitali ya Sumve (VAH), ambayo ipo umbali wa kilomita moja. Serikali itaendelea kutenga bajeti, kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa na kuajiri watumishi wa kada mbalimbali za afya kwa ajili ya vituo vya kutolea huduma za afya nchini.