Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 238 2025-05-07

Name

Jonas William Mbunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbinga Mjini

Primary Question

MHE. JONAS W. MBUNDA aliuliza:-

Je, lini ujenzi wa maboma ya madarasa, nyumba za walimu na vyoo kwenye shule za msingi na sekondari Halmashauri ya Mbinga utakamilika?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Mji Mbinga ina jumla ya maboma 88 yakijumuisha maboma ya madarasa 29 na matundu ya vyoo 59 kwa shule za msingi na sekondari ambapo jumla ya shilingi milioni 329.8 zinahitajika ili kukamilisha maboma haya.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika Mwaka wa Fedha 2024/2025, Serikali ilitenga shilingi 180,000,000 kwa ajili ya kukamilisha maboma tisa ya madarasa na matundu 30 ya vyoo, ambapo hadi Machi, 2025 shilingi milioni 79.98 zimetolewa kukamilisha maboma sita ya madarasa na matundu 30 ya vyoo katika Shule za Msingi Chemka, Kipungu, Kindimba, Torongi na Kitunda shule Shikizi, Masasi, Lusewa Shule Shikizi, Lupilo, Rudisha, Mpepai, Kitete na Lazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetenga shilingi 120,000,000 kwa ajili ya kukamilisha maboma manne ya madarasa na matundu 41 ya vyoo katika Shule za Halmashauri ya Mji wa Mbinga. Aidha, Serikali itaendelea kukamilisha maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi kwa awamu. Ahsante.