Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 228 2025-05-06

Name

Emmanuel Peter Cherehani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ushetu

Primary Question

MHE. EMMANUEL P. CHEREHANI aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza mgogoro wa mpaka wa Shinyanga na Tabora katika eneo la Ushetu na Kaliua ambao umechukua muda mrefu sana?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa tafsiri ya ardhini ya Matangazo ya Serikali ya uanzishwaji wa Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga na Kaliua Mkoani Tabora, hakuna mgogoro wa mpaka kati ya mikoa hiyo miwili. Mgogoro uliopo wa mpaka ni kati ya Hifadhi ya Msitu wa Mto Igombe unaomilikiwa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) na msitu wa Hifadhi wa Ushetu Ubagwe unaomilikiwa na Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu.

Mheshimiwa Mwenyekiti, mgogoro huo umetokana na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kuweka alama za mipaka kwenye eneo la Hifadhi ya Msitu wa Ushetu Ubagwe uliopo kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ushetu Mkoani Shinyanga.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa mujibu wa Matangazo ya Serikali ya uanzishwaji wa Hifadhi ya Msitu wa Igombe River, Tangazo la Serikali Na. 32 la mwaka 1958 na Hifadhi ya msitu wa Ushetu Ubagwe, Tangazo la Serikali Na. 442 la mwaka 1958 hakuna mwingiliano wa mipaka kati ya hifadhi hizi mbili.

Mheshimiwa Mwenyekiti, Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) itaendelea kuhakikisha Hifadhi ya Msitu wa Igombe River inabakia kwenye mipaka yake kama ilivyo kwenye Tangazo la Serikali Na. 32 la mwaka 1958 la uanzishwaji wa hifadhi hiyo.