Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 239 2025-05-07

Name

Felista Deogratius Njau

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FELISTA D. NJAU aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga uzio katika Kituo cha Afya cha Uru Kusini - Moshi Vijijini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2021/2022, Serikali imepeleka jumla ya shilingi milioni 750 katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha afya cha Uru Kusini ambapo majengo matano ujenzi umekamilika na kituo hicho kinatoa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2026/2027, Serikali kupitia mapato ya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Moshi itatenga shilingi milioni 50 kwa ajili ya ujenzi wa uzio wa Kituo cha afya Uru Kusini. Ahsante.