Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 240 2025-05-07

Name

Innocent Edward Kalogeris

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Morogoro Kusini

Primary Question

MHE. INNOCENT E. KALOGERIS aliuliza:-

Je, lini Serikali itaipatia Gari la Wagonjwa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022 ilinunua magari 594 ya kubebea wagonjwa na usimamizi wa huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Wilaya ya Morogoro ilipokea magari matatu ya kubebea wagonjwa na kupelekwa Vituo vya Afya Duthumi, Mkuyuni na Ngerengere.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa dharura zinazotokea katika Hospitali ya Wilaya ya Morogoro zinashughulikiwa na gari lililopo kwenye Kituo cha Afya cha Duthumi kilichopo takribani umbali wa kilometa 20.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inaendelea kutenga bajeti ya kununua magari ya wagonjwa kwa ajili ya hospitali za halmashauri kote nchini ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Morogoro. Ahsante. (Makofi)