Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 19 | Sitting 18 | Enviroment | Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira na Muungano | 229 | 2025-05-06 |
Name
Jacqueline Kandidus Ngonyani (Msongozi)
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JACQUELINE N. MSONGOZI aliuliza:-
Je, Serikali imejipangaje kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ambayo yanachangia uharibifu wa mazingira?
Name
Khamis Hamza Khamis
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Uzini
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO NA MAZINGIRA alijibu:-
Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imeandaa sera, mikakati, kanuni, miongozo na mipango ya kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi: Sera ya Taifa ya Mazingira (2021); Mkakati wa Taifa wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (2021-2026); Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (2022–2032); na Kanuni za Marekebisho ya Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa Biashara ya Kaboni za mwaka 2023 ambazo zinasomwa pamoja na Kanuni za Udhibiti na Usimamizi wa Biashara ya Kaboni za mwaka 2022.
Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, Serikali imendeelea kuwahamasisha wananchi kuacha shughuli zinazochangia uharibifu wa mazingira, zikiwemo kukata miti ovyo, kuepuka kilimo kisicho endelevu katika vyanzo vya maji, kuepuka ufugaji unaochangia uharibifu wa mazingira na uvuvi haramu. Aidha, kuachana na matumizi ya nishati ya kuni na mkaa kwa taasisi zinazolisha watu zaidi ya 100 na kuhamia katika matumizi ya nishati safi ya kupikia ili kuweza kuchangia katika utunzaji wa mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved