Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Regional Administration and Local Government Authorities Ofisi ya Rais TAMISEMI. 241 2025-05-07

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. FLATEI G. MASSAY K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza:-

Je, lini Serikali itapeleka Gari la Wagonjwa kwenye Kituo cha Afya cha Mgori Jimbo la Singida Kaskazini?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika mwaka wa fedha 2021/2022, ilinunua magari 594 ya kubebea wagonjwa na usimamizi wa huduma za afya katika Mamlaka za Serikali za Mitaa. Halmashauri ya Wilaya ya Singida imepokea magari mawili ya kubebea wagonjwa na kupelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Singida na Kituo cha Afya cha Mgori.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa awamu kwa ajili ya ununuzi wa magari ya kubebea wagonjwa na kuyapeleka katika halmashauri kote nchini kwa ajili ya kutoa huduma kwenye hospitali na vituo vya afya. Ahsante. (Makofi)