Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 230 2025-05-06

Name

Jacquline Andrew Kainja

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. VENANT D. PROTAS K.n.y. MHE. JACQUELINE K. ANDREA aliuliza: -

Je, lini Serikali itamaliza kusambaza umeme kwenye vitongoji vyote nchini?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu: -

Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) imekamilisha kupeleka umeme katika vitongoji 33,657 kati ya vitongoji 64,359 vilivyopo nchini. Aidha, vitongoji 30,702 bado havijafikiwa na huduma ya umeme, ambapo kati ya hivyo, vitongoji 7,736 tayari vipo katika hatua ya utekelezaji kupitia miradi mbalimbali; na vitongoji vilivyosalia 22,966 vitapatiwa umeme kwa kipindi cha miaka mitano kulingana na upatikanaji wa fedha, ahsante.