Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 232 2025-05-06

Name

Tumaini Bryceson Magessa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Busanda

Primary Question

MHE. TUMAINI B. MAGESSA aliuliza: -
Je, ujenzi wa Barabara ya Mpomvu kupitia Nyarugusu kwenda Bulyankulu kwa kiwango cha lami upo katika hatua gani?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Barabara ya Mpomvu – Nyarugusu inajulikana kwa jina la Geita – Bukoli – Bulyankulu Junction (Ilogi) yenye urefu wa kilometa 61.2. Kwa sasa Serikali iko katika hatua za mwisho za manunuzi ya Mkandarasi kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami, ahsante. (Makofi)