Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 242 2025-05-07

Name

Stephen Lujwahuka Byabato

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bukoba Mjini

Primary Question

MHE. STEPHEN L. BYABATO aliuliza:-

Je, kwa nini watumishi wanaojitolea wanapoajiriwa wasipangiwe katika Vituo walivyokuwa wakijitolea kama kipaumbele cha kwanza?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu ya Sera ya Menejimenti na Ajira katika Utumishi wa Umma, Toleo Na.2 la Mwaka 2008, ikisomwa pamoja na Sheria ya Utumishi wa Umma, Sura 298, Ajira katika Utumishi wa Umma hupatikana kwa ushindani na uwazi. Kujitolea katika Utumishi wa Umma huwezesha vijana kujipatia ujuzi wa ziada pamoja na kuwapa uzoefu na uwezo wa kushindana pindi ajira zinapotangazwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, pale ambapo wanaojitolea wanafaulu usaili, majina yao hupelekwa kwa waajiri ambao huwapangia vituo vya kazi kulingana na mahitaji ya ikama iliyoidhinishwa katika vituo husika. Ninakushukuru.