Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 233 2025-05-06

Name

Vita Rashid Kawawa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Namtumbo

Primary Question

MHE. VITA R. KAWAWA aliuliza: -

Je, kwa nini ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma umesimama?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma unatekelezwa kwa awamu ambapo hadi sasa Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi bilioni 3.3 na tayari jengo la huduma za mionzi limekamilika sambamba na kusimikwa mashine ya CT-Scan na Digital X-Ray na tayari huduma zinatolewa. Aidha, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) unaendelea na jengo la kusafisha figo (Dialysis).

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha 2024/2025 Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi bilioni mbili kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Ruvuma, na mradi huu unatarajiwa kukamilika katika awamu tatu.