Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Energy and Minerals Wizara ya Nishat 243 2025-05-07

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA aliuliza:-

Je, lini majiko yanayotumia gesi yataanza kutumika katika Shule za Sekondari kote Nchini?

Name

Judith Salvio Kapinga

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer


NAIBU WAZIRI WA NISHATI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, hadi kufikia mwezi Machi, 2025, Serikali kupitia wadau mbalimbali imewezesha jumla ya shule za sekondari 216 kuhamia katika matumizi ya nishatisafi ya kupikia ambapo kati ya hizo, shule za sekondari 146 zinatumia Gesi ya LPG. Aidha, Serikali kupitia REA inaendelea kutoa ruzuku ya ujenzi wa miundombinu ya nishati safi ya kupikia kwa shule nyingine.

Mheshimiwa Naibu Spika, tarehe 20 Aprili, 2025, REA kupitia Wizara ya Nishati imepokea kibali kutoka TAMISEMI cha kufunga miundombinu ya huduma ya nishati safi ya kupikia katika shule 115 zikiwemo: shule za mikoa za sayansi za wasichana 16; shule za kitaifa za wavulana 7; shule za bweni za kawaida 66; na shule kongwe za sekondari 26. Serikali kupitia REA na wadau mbalimbali itaendelea kufunga miundombinu ya nishati ya kupikia katika shule za sekondari kulingana na upatikanaji wa fedha. Ahsante.