Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 244 2025-05-07

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza:-

Je, lini NHIF itajumuisha huduma za afya ya akili kwenye vifurushi vya bima ya afya?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, huduma za matibabu ya afya ya akili, ushauri nasaha na huduma nyingine za kibingwa ikiwemo huduma za utengamao ni baadhi ya huduma zilizoorodheshwa kama huduma muhimu za afya kwenye mwongozo wa matibabu (Standard Treatment Guideline) ambapo hutumika kama kigezo kikuu cha huduma za msingi zinazolipiwa na Mfuko wa Bima ya Afya wa Taifa.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika utoaji wa huduma za matibabu kwa wagonjwa wa akili, Mfuko wa Bima (NHIF) hugharamia dawa zote kwa kuzingatia aina ya dawa na ngazi ya huduma kwa mujibu wa Mwongozo wa Matibabu (STG).