Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 18 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 234 2025-05-06

Name

Angelina Adam Malembeka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ANGELINA ADAM MALEMBEKA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kurejesha kilimo cha pamba katika Mikoa ya Kusini mwa Tanzania?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Mikoa ya Kusini mwa Tanzania ikiwemo Mkoa wa Mtwara, Lindi, Rukwa, Songwe, Mbeya, Njombe na Ruvuma hairuhusiwi kulima pamba kutokana na karantini iliyowekwa kufuatia uwepo wa funza mwekundu. Karantini hiyo iliwekwa tangu mwaka 1947 na kuhuishwa mwaka 2000 baada ya wakulima wa Halmashauri ya Chunya Mkoani Mbeya kuripoti uwepo wa funza huyo ambaye alisababisha uharibifu wa pamba kwa 100%.

Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, utafiti uliofanyika mwaka 2022 katika mikoa yenye karantini ulithibisha kuwa funza mwekundu bado yupo katika maeneo hayo. Hivyo, mikoa hiyo bado haijaruhusiwa kurejesha kilimo cha pamba kwa lengo la kudhibiti kusambaa kwa funza huyo katika maeneo mengine ya uzalishaji wa pamba nchini.

Mheshimiwa Mwenyekiti, wakulima katika maeneo yaliyowekewa karantini wanashauriwa kuendelea kulima mazao mengine ikiwemo korosho, ufuta, alizeti, chai, mihogo, mahindi na mbaazi kulingana na ekolojia ya maeneo waliyopo. (Makofi)