Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 245 2025-05-07

Name

Dr. Thea Medard Ntara

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:-

Je, upi mkakati wa kuzirudishia Hospitali za Mafunzo Vyuo Vikuu vyenye Programu ya Afya kama UDOM na MUHAS ili kukidhi miongozo ya Kimataifa?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali iliipa Wizara ya Afya jukumu la kusimamia Hospitali ya Mloganzila na Benjamin Mkapa ambazo zilikuwa Hospitali za Vyuo Vikuu vya MUHAS na UDOM, kwa lengo la kuimarisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi sambamba na kuboresha ubora wa huduma.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa sasa Vyuo Vikuu vya Dodoma na Muhimbili vinaendelea kutumia Hospitali hizi kufundishia wanafunzi wao. Ninaomba kuwasilisha.