Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 246 2025-05-07

Name

Dr. Paulina Daniel Nahato

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. DKT. PAULINA D. NAHATO aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Taasisi na Mashirika yanatoa fursa kwa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kufanya mazoezi kwa vitendo?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKINOLOJIA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuhakikisha wanafunzi wanapata fursa za kufanya mafunzo kwa vitendo, vyuo vikuu nchini vimekuwa na utaratibu wa kuanzisha ushirikiano na taasisi na mashirika ambayo yanatoa huduma zinazoshabihiana na fani zinazotolewa vyuoni. Hadi sasa taasisi 19 za elimu ya juu zimeanzisha Kamati za Ushauri wa Kitasnia (Industrial Advisory Commitee) kama mkakati wa kuongeza nafasi na kuimarisha mafunzo kwa vitendo ambapo jumla ya mikataba 158 imesainiwa kati ya vyuo na taasisi binafsi na viwanda. Ninakushukuru sana.