Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 247 2025-05-07

Name

Mustafa Mwinyikondo Rajab

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Dimani

Primary Question

MHE. MUSTAFA MWINYIKONDO RAJAB aliuliza:-

Je, Idara ya Uhamiaji ina mpango gani wa kujenga hospitali Zanzibar kama ilivyo kwa Vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo kwa vyombo vingine vya Ulinzi na Usalama, Idara ya Uhamiaji ina mpango wa kuwa na zahanati kwa lengo la kutoa huduma za afya kwa watumishi na jamii inayoizunguka. Serikali kupitia Idara ya Uhamiaji imefanya mawasiliano ya awali na Wizara ya Afya ya Zanzibar ili kupata mwongozo kuhusu namna bora ya uanzishwaji wa zahanati itakayokidhi mahitaji kwa jamii itakayohudumiwa. Ahsante.