Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 19 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 248 2025-05-07

Name

Omar Issa Kombo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wingwi

Primary Question

MHE. OMAR ISSA KOMBO aliuliza:-

Je, lini Serikali itajenga kituo kipya cha Polisi cha Wilaya ya Micheweni?

Name

Daniel Baran Sillo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Babati Vijijini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itajenga Kituo Kipya cha Polisi cha Daraja “B” katika Wilaya ya Micheweni, ambacho kitagharimu kiasi cha fedha shilingi 802,926,788, kwa kuwa kituo kilichopo sasa ni chakavu na hakiwezi kufanyiwa ukarabati. Mpango wa ujenzi wa kituo kipya unaanza kwenye mwaka wa fedha 2024/2025 kupitia Mfuko wa Tuzo na Tozo, ahsante.