Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2015-2020 Session 16 Sitting 5 Information, Culture, Arts and Sports Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo 64 2019-09-09

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA aliuliza:-

(a) Je, ni sababu zipi zinazosababisha matangazo ya Shirika la Habari Tanzania (TBC) hasa upande wa Radio yasisikike kwenye Tarafa za Kitunda na maeneo mengi ndani ya Jimbo la Sikonge?

(b) Je, ni lini Serikali itarekebisha tatizo hilo?

Name

Juliana Daniel Shonza

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa ruhusa yako kwanza naomba nitumie fursa hii kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuipongeza Timu yetu ya Taifa, Taifa Stars, kwa kutuheshimisha sisi kama Taifa kwa kuitoa Timu ya Burundi kwa mikwaju ya penati na hatimaye kuweza kutinga kwenye hatua ya makundi.

Mheshimiwa Spika, sasa naomba nijielekeze kwenye swali; kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph George Kakunda, Mbunge wa Sikonge, lenye vipengele (a) na (b), kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, TBC kwa Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2016/2017 ilitekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika wilaya tano zilizopo mipakani mwa nchi yetu; wilaya hizo ni pamoja na Wilaya ya Longido Mkoani Arusha, Wilaya ya Rombo Mkoani Kilimanjaro, Wilaya ya Tarime Mkoani Mara, Wilaya ya Nyasa Mkoani Ruvuma na Wilaya ya Kibondo Mkoani Kigoma. Aidha, Bajeti ya Mwaka 2017/2018 TBC ilitekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika Mkoa wa Mtwara na Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga. Hadi kufikia tarehe 04 Mei, 2019 shirika lina vituo 33 vya kurushia matangazo katika masafa ya FM kwenye wilaya 102.

Mheshimiwa Spika, TBC inaendelea na mpango wa kupanua usikivu maeneo yote ya nchi nzima, kutegemeana na upatikanaji wa fedha ili kukamilisha wilaya zote 59 ikiwepo Wilaya ya Sikonge. Aidha, TBC ina mpango wa kufanya maboresho katika mitambo yake iliyopo Tabora Kaze Hill kisha kufanya tathmini ya usikivu na kubainisha maeneo yanayopaswa kufungiwa mitambo mingine ili kuleta usikivu Mkoa mzima wa Tabora ikiwepo Wilaya ya Sikonge.

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya Mwaka wa Fedha 2019/2020, TBC inaendelea kutekeleza mradi wa upanuzi wa usikivu katika maeneo ya Mikoa ya Unguja, Pemba, Simiyu, Njombe, Songwe pamoja na Lindi. Mkakati wa Serikali ni kuiwezesha TBC kufikia usikivu katika maeneo yote ya Tanzania.