Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 3 Sitting 44 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 372 2021-06-04

Name

Husna Juma Sekiboko

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza:-

Je, ni lini Serikali itafanya marekebisho ya malengo ya Mtaala wa Elimu ya Msingi na Sekondari nchini ili kuendana na uhitaji wa sasa?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Husna Juma Sekiboko Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kufanyia marekebisho mitaala ya elimu ya msingi na sekondari ili kuwawezesha wanafunzi kupata stadi mbalimbali zinazoendana na mahitaji ya wakati. Kwa sababu hiyo, Serikali imekuwa ikiboresha mitaala hiyo kila kunapokuwa na hitaji la kisayansi, kisiasa, kiuchumi, kiutamaduni na kiteknolojia.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022 Serikali imepanga kufanya mjadala mpana kuhusu mfumo wa Elimu nchini ambao utahusisha Sera ya Elimu na Mitaala kwa ujumla ili iendane na wakati na ikidhi mahitaji ya sasa na baadaye. Ahsante.