Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 8 | Sitting 2 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 38 | 2022-09-14 |
Name
Omar Ali Omar
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Wete
Primary Question
MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: -
Je, wanafunzi wangapi kutoka Zanzibar wamepata mikopo ya elimu ya juu kwa mwaka 2020/2021?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia napenda sasa kujibu swali la Mheshimiwa Omar Ali Omar, Mbunge wa Wete kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu imekuwa ikitoa mikopo kwa wanafunzi wote wa Kitanzania wenye uhitaji bila kuangalia mwombaji anatoka upande upi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Mheshimiwa Spika, hata hivyo, takwimu za mwaka 2020/2021 zinaonesha kuwa wanafunzi Watanzania wapatao 1,492 wanaosoma katika taasisi sita za elimu ya juu zilizopo Zanzibar walipangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.3. Aidha, kwa mwaka 2021/2022 jumla ya wanafunzi wa Tanzania 1,929 wanaosoma katika taasisi za elimu ya juu Zanzibar walipangiwa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 5.8. Nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved