Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 2 | Policy, Coordination and Parliamentary Affairs | Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge | 21 | 2022-11-02 |
Name
Abdallah Jafari Chaurembo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbagala
Primary Question
MHE. ABDALLAH J. CHAUREMBO aliuliza: -
Je, nini kauli ya Serikali juu ya mapunjo ya fidia kwa wananchi walioathirika na mlipuko wa mabomu Mbagala?
Name
George Boniface Simbachawene
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kibakwe
Answer
WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE NA URATIBU) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Abdallah Jafari Chaurembo, Mbunge wa Mbagala, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa mkono wa pole na siyo fidia, kwa wananchi 12,647 waliothirika na milipuko ya mabomu iliyotokea tarehe 29 Aprili, 2009 katika Kambi ya JWTZ Mbagala. Malipo hayo, yalitolewa kwa awamu sita kuanzia mwaka 2009 hadi 2020. Vile vile, Serikali ilitoa kifuta machozi pamoja na kugharamia huduma za mazishi kwa familia 29 zilizopoteza wapendwa wao kutokana na milipuko hiyo ya mabomu ya Mbagala.
Mheshimiwa Spika, zoezi la kutoa mkono wa pole kwa waathirika lilisitishwa rasmi na Serikali mnamo mwezi Machi, 2020 baada ya walengwa wote waliokusudiwa kujitokeza na kulipwa.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved