Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 3 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 24 | 2022-04-08 |
Name
Nusrat Shaaban Hanje
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza: -
Je? Serikali ina mkakati gani wa kuzuia ukatali wa kijinsia na utumikishwaji wa watoto katika makambi yanayotarajiwa kujengwa ili kuwezesha ujenzi wa Bomba la Mafuta Hoima Tanga?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ahsante. Napenda kujibu swali la Mheshimiwa Nusrat Shaaban Hanje, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia na utumikishaji wa watoto vinakomeshwa katika maeneo mbalimbali nchini ikiwemo mradi wa bomba la mafuta Hoima Tanga, kupitia MTAKUWWA Wizara yangu imejipanga kuimarisha na kuzijengea uwezo Kamati za Ulinzi na Usalama kwa watoto kwa vile Serikali itaendelea kutumia vyombo vya dola kuhakikisha wale wote wanaotumikisha watoto na kufanya vitendo vya ukatili wanachukuliwa hatua za kisheria. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved