Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 9 | Sitting 9 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 134 | 2022-11-10 |
Name
Francis Isack Mtinga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Iramba Mashariki
Primary Question
MHE. FRANCIS I. MTINGA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Mahakama ya Wilaya katika Halmashauri ya Mkalama?
Name
Geophrey Mizengo Pinda
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kavuu
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, ahsante, kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria napenda kujibu swali la Mheshimiwa Francis Isack Mtinga, Mbunge wa Iramba Mashariki, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Mahakama ya Tanzania inaendelea kutekeleza mpango wake wa kuhakikisha kuwa kila Wilaya inakuwa na jengo la Mahakama. Aidha kwa sasa miradi inayoendelea ni ujenzi wa majengo ya Mahakama za Wilaya 18. Ujenzi wa Jengo la Mahakama ya Wilaya ya Mkalama umepangwa kufanyika katika mwaka huu wa fedha 2022/2023. Kwa sasa taratibu za kumpata Mkandarasi wa ujenzi zinaendelea. Ahsante. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved