Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 10 | Sitting 1 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 10 | 2023-01-31 |
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kudhibiti madalali wanaodalalia mazao ya wananchi yakiwa shambani kwa bei wanazozitaka?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Saashisha Elinikyo Mafuwe Mbunge wa Jimbo la Hai kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inatekeleza mpango wa uanzishwaji wa vituo rasmi vya uuzaji na ununuzi wa mazao ya kilimo karibu na maeneo ya uzalishaji ili kumuwezesha mkulima kuuza mazao yake kwa bei ya soko na kuzuia uuzwaji wa mazao shambani. Vilevile Serikali inaendelea na mpango wa ujenzi wa ghala za kuhifadhia mazao katika maeneo ya uzalishaji ili kuwezesha wakulima kuhifadhi na kuuza mazao yao.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved