Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 7 | Sitting 23 | Foreign Affairs and International Cooperation | Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki | 204 | 2022-05-16 |
Name
Ussi Salum Pondeza
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chumbuni
Primary Question
MHE. ABDUL-HAFAR IDRISSA JUMA K.n.y. MHE. USSI SALUM PONDEZA aliuliza: -
Je, ni nchi ngapi zimeshafungua Ofisi zao za Ubalozi Jijini Dodoma baada ya zoezi la kuhamisha Makao Makuu ya Serikali Dodoma?
Name
Amb. Liberata Rutageruka Mulamula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Nominated
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Pondeza Mbunge wa Chumbuni, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, hadi sasa nchi tatu zimeshafungua Ofisi Ndogo za Ubalozi Jijini Dodoma. Nchi hizo ni Uingereza, Ujerumani na China. Hata hivyo, Wizara inaendelea kuzishawishi nchi nyingine kufungua Ofisi zao hapa Jijini Dodoma.
Mheshimiwa Spika, katika hatua nyingine baadhi ya Mashirika ya huduma za jamii na maendeleo ya Umoja wa Mataifa yameshafungua Ofisi zake Jijini Dodoma. Mashirika hayo ni pamoja na UNDP, UNICEF, UN Women, WFP, WHO, UNFPA, FAO, IFAD, IOM, UNAID, UNCDF na UNIDO.
Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved