Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 11 Sitting 1 Education, Science,Technology and Vocational Training, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia 11 2023-04-04

Name

Nusrat Shaaban Hanje

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. NUSRAT S. HANJE aliuliza: -

Je ni lini Serikali itatoa mikopo kwa wanafunzi wa Vyuo vya Kati nchini?

Name

Omary Juma Kipanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mafia

Answer

NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia naomba kujibu Swali la Mheshiwa Nusrat Shaaban Hanje, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa elimu ya kati katika maendeleo ya nchi, Serikali imeendelea kugharamia uendeshaji wa vyuo vya kati kupitia ruzuku ambapo kwa mwaka 2022/2023, imetenga kiasi cha shilingi Bilioni 41.47 kwa wanafunzi 2,435 waliopo katika vyuo vya kati wanaosoma fani za sayansi na ufundi. Aidha, Serikali inakamilisha taratibu za kuwezesha mikopo kutolewa kwa ajili ya elimu ya kati.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana.