Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 6 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 70 | 2023-04-13 |
Name
Issa Ally Mchungahela
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Lulindi
Primary Question
MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA aliuliza: -
Je, Serikali haioni haja ya kuwa na Chuo cha VETA katika kila Jimbo ili kuwakomboa vijana na tatizo la ajira?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Issa Ally Mchungahela, Mbunge wa Jimbo la Lulindi, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa sasa, azma ya Serikali ni kujenga Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) katika kila Mkoa na Wilaya nchini. Katika mwaka wa fedha 2022/2023, Serikali imetenga kiasi cha shilingi bilioni 100 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa vyuo vya VETA katika Wilaya 63 ambazo hazina vyuo hivyo. Kiasi hiki pia kitatumika katika ujenzi wa Chuo cha VETA cha Mkoa wa Songwe ambao hauna chuo cha ngazi hiyo.
Mheshimiwa Spika, kwa sasa, Serikali inaendelea kutekeleza azma hiyo na ikishakamilisha ujenzi wa VETA katika kila Wilaya itaangalia uwezekano wa kuanza kujenga vyuo hivyo katika Majimbo kulingana na uhitaji na upatikanaji wa fedha. Ninakushukuru sana. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved