Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 6 | Works, Transport and Communication | Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi | 74 | 2023-04-13 |
Name
Mrisho Mashaka Gambo
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Arusha Mjini
Primary Question
MHE. MRISHO M. GAMBO aliuliza:-
Je, lini Wananchi wa Kata ya Moshono katika barabara ya mzunguko ya Kona ya Kiserian watalipwa fidia?
Name
Atupele Fredy Mwakibete
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Busokelo
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI (MHE. ATUPELE F. MWAKIBETE) alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mrisho Mashaka Gambo, Mbunge wa Arusha Mjini, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuwalipa fidia wananchi walioathirika na kupisha ujenzi wa barabara ya mzunguko (Arusha bypass) kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved