Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 12 | Sitting 7 | Community Development, Gender and Children | Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum | 99 | 2023-09-06 |
Name
Janeth Elias Mahawanga
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. JANETH E. MAHAWANGA aliuliza:-
Je, nini mpango wa kuhakikisha Majukwaa ya Kuwezesha Wanawake Kiuchumi yanaleta tija kwenye mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri?
Name
Mwanaidi Ali Khamis
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Elias Mahawanga, Viti Maalum, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Majukwaa ya Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi yameleta tija kwenye asilimia 10 ya Halmashauri ya kuwezesha kuunda vikundi vya kiuchumi ambavyo hukutanisha wanawake katika ngazi zote za jamii ili kujadili fursa, changamoto na jinsi ya kushiriki katika shughuli za kiuchumi hususan biashara, kilimo, madini, ujenzi, uchukuzi, usindikaji wa maliasili na mazao ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika jamii, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved