Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 36 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 474 | 2023-05-30 |
Name
Venant Daud Protas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igalula
Primary Question
MHE. VENANT D. PROTAS aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itajenga Chuo cha VETA katika Jimbo la Igalula?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Naomba kujibu Swali la Mheshimiwa Venant Daud Protas Mbunge wa Jimbo la Igalula kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali inatambua umuhimu wa vyuo vya ufundi stadi katika kuwasaidia wananchi kupata ujuzi utakao wasaidia kutekeleza kazi zao za kiuchumi. Kwa sasa Serikali inatekeleza azma ya kujenga chuo cha ufundi stadi katika kila mkoa na wilaya nchini.
Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Igalula lipo katika Wilaya ya Uyui na kwa sasa Serikali inakamilisha ujenzi wa Chuo cha Wilaya ya Uyui. Ujenzi huo umefikia asilimia 97 na chuo hiki kimeshaanza kutoa mafunzo ya muda mfupi.
Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya kukamilisha ujenzi wa vyuo vya VETA katika wilaya zote nchini, Serikali itaangalia uwezekano wa kujenga vyuo vya VETA katika ngazi za majimbo na ngazi zingine za chini kadri ya upatikanaji wa fedha na uhitaji, nakushukuru.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved