Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 39 | Education, Science,Technology and Vocational Training, | Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia | 510 | 2023-06-02 |
Name
Omar Ali Omar
Sex
Male
Party
ACT
Constituent
Wete
Primary Question
MHE. OMAR ALI OMAR aliuliza: -
Je, kwa nini Serikali haipangi kusahihishia mitihani ya kidato cha nne Zanzibar?
Name
Omary Juma Kipanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mafia
Answer
NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Omari Ali Omari, Mbunge wa Wete, kama ifuatavyo;
Mheshimiwa Spika, kwa mwaka 2021 na 2022 Serikali ilisahihisha mitihani ya Taifa, kidato cha nne (CSEE) katika kituo cha Shule ya Sekondari Hasnuu Makame, Kusini Unguja. Aidha, Serikali itaendelea kusahihisha mitihani Zanzibar kwa vituo vya mitihani vyenye sifa za kulaza watahini wasiopungua 500 kwa wakati mmoja, kuwa na vyumba visivyopungua ishirini vya kazi, na miundombinu ya maji na umeme kwa wakati wote wa kazi ya kusahihisha, nakushukuru sana.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved