Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
---|---|---|---|---|---|---|
2020-2025 | Session 11 | Sitting 47 | Justice and Constitutional Affairs | Wizara ya Katiba na Sheria | 613 | 2023-06-13 |
Name
Japhet Ngailonga Hasunga (CPA)
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Vwawa
Primary Question
MHE. JAPHET N. HASUNGA aliuliza:-
Je, lini Serikali itatenga fedha na kuanza ujenzi wa Mahakama ya Mkoa wa Songwe?
Name
Pauline Philipo Gekul
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Babati Mjini
Answer
NAIBU WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria naomba sasa nijibu swali la Mheshimiwa Japhet Ngailonga Hasunga, Mbunge wa Vwawa, kama ifuatavyo:-
Mheshimiwa Naibu Spika, ujenzi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Songwe ulianza katika mwaka wa fedha 2021/2022, na jengo hilo lilijengwa eneo la Vwawa Wilayani Mbozi na lilikamilika Julai, 2022. Aidha, Jengo lilianza kutumika Agosti, 2022 na kuzinduliwa rasmi na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania mwezi Novemba, 2022 ambapo alizindua kwa pamoja na majengo ya Mahakama za Hakimu Mkazi katika Mikoa ya Lindi na Katavi, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2024. All Rights Reserved